Coat of Arms

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa

“ Kituo Cha Fursa ”

KSW Logo
Bigwa FDC
Karibu Bigwa Folk Development College

Kuhusu Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa

Kituo cha umahiri kinacholenga kuwajengea wananchi maarifa, stadi na uwezo wa kujiletea maendeleo endelevu.

Dhana ya Elimu ya Maendeleo ya Wananchi

Elimu ya Maendeleo ya Wananchi ni elimu inayotolewa kwa mwananchi ili kumuwezesha kupata maarifa, ujuzi na umahiri katika matumizi ya rasilimali zilizopo na kutawala mazingira ili kuleta maendeleo ya haraka kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

🎯

Dira

Kuwa Chuo kinachoongoza katika utoaji wa ujuzi kulingana na mahitaji ya jamii nchini Tanzania na Afrika Mashariki.

🚀

Dhima

Kusimamia na kushauri kuhusu utoaji wa ujuzi kulingana na mahitaji ya jamii kwa kutumia mitaala husika.

Historia ya Chuo

Historia Fupi ya CMW Bigwa

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa (CMW Bigwa) ni miongoni mwa vyuo hamsini na nne vilivyoanzishwa mwaka 1975 kutokana na wazo la Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere baada ya kutembelea Sweden na kuona mfumo wa Folk High Schools.

Kilianzishwa kama sehemu ya awamu ya tatu ya Elimu ya Watu Wazima yenye lengo la kuwajengea wananchi maarifa, stadi na uwezo wa kujitegemea.

Uamuzi wa kuanzishwa kwa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi ulitokana na Waraka wa Baraza la Mawaziri Na. 96 wa mwaka 1974. Hadi mwaka 1978 jumla ya vyuo 53 vilikuwa vimeanzishwa nchini.

Bigwa ni miongoni mwa vyuo vinne vilivyojengwa mahsusi kutekeleza maono ya Baba wa Taifa mwaka 1975 pamoja na Sengerema, Ngara na Handeni.

Takwimu

8 Fani zinazotolewa
25 Watumishi
380+ Wanafunzi
10,000+ Wahitimu